News & Updates

Wizara ya Viwanda na Biashara Yaunga Mkono Consumer Choice Awards, Yathibitisha Ushiriki Dubai

News & Updates

Wizara ya Viwanda na Biashara imepongeza na kutoa baraka zake kwa tuzo za Consumer Choice Awards, ikieleza kuwa jukwaa hilo lina umuhimu mkubwa katika kutangaza biashara, uwekezaji na fursa mbalimbali za kiuchumi za Tanzania.

Wizara hiyo kupitia Katibu Mkuu Waziri Salum, imeeleza kuwa uwepo wa tuzo hizo unatoa nafasi kwa sekta binafsi na Wadau mbalimbali kutambulika zaidi ndani na nje ya Nchi, hususan kupitia shughuli zinazofanyika katika majukwaa ya Kimataifa.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Consumer Choice Awards, Dkt. Diana Laizer, amesema Waziri ameonesha kufurahishwa baada ya kuona taarifa na video kuhusu tuzo hizo kupitia mitandao ya kijamii, ikiwemo shughuli zinazofanyika Dubai, na kuwa tuzo hizo ni jukwaa kubwa linaloweza kusaidia kuitangaza Tanzania, kukuza uwekezaji na kuendeleza shughuli zinazohusiana na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Aidha, Dkt. Laizer amesema Waziri pia amewapongeza kwa kuanzisha wazo hilo, akieleza kuwa ni wazo lenye manufaa si kwa waandaaji pekee, bali kwa taifa kwa ujumla. Aidha, amesema Serikali kupitia Wizara hiyo imetoa dhamira ya kushirikiana na Consumer Choice Awards kwa ukamilifu, huku Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakithibitisha ushiriki wao katika tuzo hizo, zinazofanyika Novemba mwaka huu Jijini Dubai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

We take processes apart, rethink, rebuild, and deliver them back working smarter than ever before.